Mkuu wa Wilaya ya Rorya Mh. Juma I. Chikoka ameongoza ugawaji wa Vitambulisho vya Taifa (NIDA) 85,000 (Elfu themanini na tano) kwa Maafisa Watendaji wa Kata 26 za Wilaya ya Rorya.
Huu ni Utekelezaji wa Mpango wa Serikali kupitia Ofisi ya Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) kupatia Wananchi wake huduma ya Vitambulisho vya Taifa.
Uzinduzi rasmi wa Ugawaji wa Vitambulisho hivyo utafanywa na Mh. Mkuu wa Wilaya kesho tarehe 19 Oktoba, 2023 kata ya Mkoma-Shirati katika Ofisi ya Mtendaji wa kata ya Mkoma.
EWE MWANANCHI WA MKOMA FIKA KATIKA OFISI ZA MTENDAJI WA KATA YA MKOMA (karibu na kituo cha polisi Shirati) UWEZE KUPOKEA KITAMBULISHO CHAKO CHA NIDA.
Wananchi wa Kata zingine mnaelekezwa kufika Ofisi za kata zenu ili kupata utaratibu wa kupata Kitambulisho chako.
VITAMBULISHO VINAGAWIWA BURE
INGRI JUU - RORYA
Sanduku la Posta: 250 TARIME
Simu ya Mezani: 0282985583
Simu ya Mkononi :
Barua Pepe za Watumishi: mkurugenzi@roryadc.go.tz
Haki Zote Zimehifadhiwa