Mradi wa ujenzi wa Hospitali ya Wilaya ya Rorya ulianza mwaka wa fedha 2018/2019.
Kwa nyakati tofauti kati ya Mwaka wa fedha 2018/2019 mpaka 2022/2023 (miaka 6) imepokea fedha kwa ajili ya ujenzi wa miundo mbinu mbalimbali ya majengo ambapo hadi kufikia sasa jumla ya fedha Tsh 3,250,000,000.00 kutoka Serikali Kuu zimeshapokelewa, na Tsh 99,649,780.00 kutoka Mapato ya Ndani zimetumika.
Mradi huu wa ujenzi wa Hospitali ya wilaya kulingana na maelekezo kutoka OR - TAMISEMI unafanyika kwa utaratibu wa ’Force Account’’ chini ya kanuni ya 167 ya Sheria ya Manunuzi ya Umma ya mwaka 2013 mbapo kamati ziliundwa kufuatana na mwongozo huo ambazo ni Kamati ya Manunuzi, Kamati ya Mapokezi, Kamati ya Ujenzi na kamati kuu ya kusimamia kazi hii.
MAPOKEZI YA FEDHA
Halmashauri ya Wilaya ya Rorya kwa Mwaka wa fedha 2018/2019 ilipokea kiasi cha shilingi 1,500,000,000.00 kwa ajili ya kuanza ujenzi wa hospitali ya wilaya. Majengo ambayo yalielekezwa kuanza kwa awamu ya kwanza ni saba (7), ambayo ni:
Mwezi Juni, 2020 Halmashauri ilipokea kiasi cha shilingi 300,000,000.00 kwa ajili ya kuendeleza ujenzi wa awamu ya kwanza.
Kwa mwaka wa fedha 2021/2022 Halmashauri ilipokea kiasi cha shilingi 800,000,000 kwa ajili ya ujenzi wa majengo manne;
Mwaka wa fedha 2021/2022 kiasi cha fedha Tsh 90,000,000 kilipokelewa kwa ajili ya ujenzi wa nyumba ya mtumishi (3 in 1) ambapo ujenzi umekamilika na watumishi wanaishi hapo.
Mwaka wa fedha 2022/2023 Hospitali ya ilipokea kiasi cha fedha Tsh 60,014,148 kutoka kwa wadau wa maendeleo (Global Fund) kwa ajili ya ujenzi wa kichomea taka na shimo la majivu ambapo ujenzi umekamilika.
UKAMILISHAJI WA MAJENGO YA MRADI NA KUANZA KWA HUDUMA
Hadi kufikia sasa (Oktoba 2023) majengo 5 kati ya saba yamekamilika na yanatumika kutoa huduma ambayo ni Jengo la wagonjwa wa nje (OPD), Jengo la Maabara, Jengo la Mama na mtoto na upasuaji, Jengo la Mionzi (Xray na Ultra sound) na Stoo ya dawa.
Jengo la ufuaji lipo hatua za ukamilishaji ikiwa imebakia kuwekwa masinki, milango na mfumo ya maji taka na maji safi, Jengo la utawala imebakia madirisha, mifumo ya maji taka,maji safi na umeme.
UTOAJI WA HUDUMA ZA MATIBABU
Mnamo Tarehe 26 mwezi Juni 2020 Hospitali ya Wilaya ya Rorya ilianza kutoa huduma mbalimbali za wagonjwa wa nje (OPD). Hii ni baada ya kukamilika kwa jengo la wagonjwa wa nje hivyo ikaonekana ni vyema kuanza huduma. Hadi kufikia sasa huduma zinaendelea ambapo wastani wa wateja 350 kwa mwezi wanahudumiwa katika huduma zifuatazo;
Huduma ya Xray na Ultra sound imeanza tayari hospitalini hapa.
Huduma za Wagonjwa wa nje yaani OPD pia zimeanza kutolewa.
INGRI JUU - RORYA
Sanduku la Posta: 250 TARIME
Simu ya Mezani: 0282985583
Simu ya Mkononi :
Barua Pepe za Watumishi: mkurugenzi@roryadc.go.tz
Haki Zote Zimehifadhiwa