Mfanyabiashara atabofya kiungio au link hapo juu atajisajili na kukamilisha uombaji. Atapata Namba ya Malipo yaani Control Number na akimaliza kufanya Malipo atapata Leseni yake kwenye Mfumo wa TAUSI popote alipo.
Leseni za vileo hutolewa kwa vipindi viwili (2) ambapo kipindi cha kwanza huanzia tarehe 1/04 hadi 30/09 na kipindi cha pili huanzia tarehe 1/10 hadi 31/03 mwaka unaofuata.
Kwa leseni zinazodhibitiwa na Mamlaka mbalimbali, Kwa mfano (TFDA, EWURA, TIRA, CRB, TILLI) n.k lazima mwombaji kuwa na cheti kutoka Mamlaka husika kabla ya kuomba leseni ya biashara.
- Jina la Biashara kama sio mtu binafsi (Certificate of Incorporation or Registration)
- Memorandum and Article of Association” kama ni Kampuni
- Kitambulisho cha Taifa, Cheti cha kuzaliwa au Hati ya kiapo kuonyesha kuwa ni Mtanzania na Mgeni Hati ya kuishi nchini daraja la “A” (Residnece Permit Class “A”).
- Hati ya kiuwakili (Power of Attorney) kama wenye hisa wote wa Kampuni wapo nje ya nchi.
- Ushahidi wa maandishi kuwa una mahali pa, kufanyia biashara (Kwa mfano hati za nyumba, mkataba wa upangishaji, risiti za malipo ya kodi za majengo au ardhi.
- Hati ya kujiandikisha kama mlipa kodi TRA (TIN).
Leseni za Biashara zimegawanyika katika makundi mawili:
Leseni hizi hutolewa na Wizara ya viwanda na Biashara ambazo ni;
i.Mfanyabiashara anapaswa awe na hati ya usajili iwapo anatumia jina la biashara (Certificate of Registration or Incorporation)
ii.Kama ni Kampuni mwombaji awe na “Memorandum of Article of Association” ambazo zinaonyesha kuwa kampuni imeruhusiwa kufanya biashara anayoiomba.
iii.Awe na mahali/ Eneo linalokubalika kwa aina ya biashara anayoiomba naisiwe vibanda vilivyopo kando kando ya barabara.
iv.Mfanyabishara aje na kivuli cha Cheti cha namba ya mlipa kodi (TIN) pamoja na kivuli cha cheti kinachoonyesha kuwa umelipa mapato kwa mujibu wa Sheria (Tax Clearance) ambavyo vyote vinatolewa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA).
v.Masharti mengine ya kupata Leseni hutegemea aina ya biashara mtu anayetaka kuanzisha eg. Mgahawa inadidi afuate taratibu zote za afya na kupima wafanyakazi wake.
vi.Hati ya Utaalamu (Professional Certifucates) kwa biashara zote za kitaalam.
Serikali ilirudisha rasmi utoaji wa ada za leseni za biashara kupitia Sheria ya Fedha na 5 ya mwaka 2011. Kutokana na marekebisho hayo, Utaratibu wa kutoa leseni za biashara bila malipo uliondolewa na kurudishwa ada ya Leseni kuanzia tarehe 30 Juni, 2013.
Kiwango cha ada ya leseni kinatofautina kulingana na aina ya biashara husika na eneo ilipo biashara hiyo. Mfano: Kiwango cha ada za Lesseni kwa Halamshauri ya Jiji na Manispaa ni tofauti na za Halamshauri ya Wilaya na maeneo ya vijijini.
Baada ya ulipaji wa ada hiyo mfanyabiashara atapatiwa Stakabadhi kwa malipo halali ya Fedha yake.
Mnyabiashara atakayekutwa anafanya biashara bila kuwa na Leseni atatozwa faini ya kuanzia Shs 50,000/= - hadi 300,000/= au apelekwe mahakamani hii imeainishwa kutoka kifungu Na. 10 (1) (b).
•Kulipia kila mwaka Lesseni ya Biashara yako kwa mujibu wa makadirio
•Ni jukumu la kila mfanyabishara kumiliki lesseni katika eneo lake la biashara na kuiweka mahala pa wazi ili kuonekana kwa urahisi.
INGRI JUU - RORYA
Sanduku la Posta: 250 TARIME
Simu ya Mezani: 0282985583
Simu ya Mkononi :
Barua Pepe za Watumishi: mkurugenzi@roryadc.go.tz
Haki Zote Zimehifadhiwa