Mhe. Omary Kipanga Naibu Waziri Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia(NW-WEST) alitembelea na kukagua ujenzi wa chuo cha VETA Rorya tarehe 26/9/2024.
Ujenzi wa majengo hayo umefikia ktk hatua mbalimbali.
Mhe. Naibu Waziri amewahakikishia wakandarasi na wananchi wa Rorya kuwa Mhe. Dr. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania atatoa fedha mwanzoni mwa mwezi Oktoba 2024 ili shughuli za ujenzi ziiendelee.
Naye Mkuu wa Wilaya Rorya Mhe. Dkt. Haule amemshukuru NW kwa kutembelea na kujionea changamoto za ujenzi wa mradi huo.
Amemwomba NW amfikishie salaam za shukrani Rais wetu mpendwa kwa kutoa fedha za kuendelea na ujenzi ili chuo hiki kiweze kutoa huduma ya mafunzo kwa vijana wa Rorya.
INGRI JUU - RORYA
Sanduku la Posta: 250 TARIME
Simu ya Mezani: 0282985583
Simu ya Mkononi :
Barua Pepe za Watumishi: mkurugenzi@roryadc.go.tz
Haki Zote Zimehifadhiwa