Wataalam wa Ardhi Halmashauri ya Rorya kwa kushirikiana na Wataalam toka Ofisi ya Kamishna wa Ardhi Mkoa wa Mara, wameanza kutoa Elimu juu ya Urasimishaji Makazi yao kwa kutumia Mfumo Mpya wa uchangiaji gharama kupitia benki ya NMB.
Akiongea katika Mafunzo hayo, Afisa Ardhi wa Haashauri ya Wilaya ya Rorya, ndugu Fredy Kyalawa amesema Wananchi wachache walikuwa na uelewa na hiyari ya kuchangia upimaji, lakini kikwazo kilikuwa ni wengi wa Wananchi hawakuweza, hivyo upimaji ulikwama.
Katika mpango huu, Makampuni ya Upimaji yatalipwa gharama na Benki ya NMB na gharama hizo zitarejeshwa na Wananchi kidogokidogo.
Tutarasimisha Makazi yaliyojengwa holela ili Wananchi wapate Hati za maeneo yao ndani ya Miezi sita, kuwa na Miundombinu ya Bararabara, Maji taka, Umeme na Wananchi kupata miliki iliyo salama ikiwemo na kukopesheka kwenye Taasisi za Kifedha kama dhamana; alisema ndugu Kyalawa.
Maeneo mengine yanayotarajiwa kunufaika hapa Wilayani ni Utegi, Majengo, Kirongwe, Nyang'ombe, Shirati (Obwere na Kabwana) na Mika.
Wananchi hao walishukuru mpango huo na kuukubali ila wapewe ushirikiano wa kila hatua.
INGRI JUU - RORYA
Sanduku la Posta: 250 TARIME
Simu ya Mezani: 0282985583
Simu ya Mkononi :
Barua Pepe za Watumishi: mkurugenzi@roryadc.go.tz
Haki Zote Zimehifadhiwa