Mh. Ng'ong'a Gerald Samwel maarufu kama GSN ni Diwani wa kuchaguliwa kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM) Kata ya Rabuor.
Mh. Ng'ong'a ndiye Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Rorya 2020-2025.
Mh. Ng'ong'a amezaliwa 1974, ni Msomi na Mbobezi katika maswala ya Usimamizi wa Miradi, Uongozi, Maendeleo ya Jamii, Mipango na Uchambuzi wa Sera.
UZOEFU KATIKA KAZI MBALIMBALI
•Amefanya kazi na Shirika la “International Youth Foundation” (IYF) kwa kufundisha Vijana Watanzania kwenye Shule mbalimbali za Sekondari na Msingi (za serikali na binafsi) hapa nchini juu ya Kujenga mtizamo wenye mwelekeo chanya.
•Amewahi kuwa Mtafiti Kiongozi na Mchambuzi wa Sera wa Uwezo Afrika Mashariki kwa miaka 6. Kama Mtafiti amezifikia wilaya zote za Tanzania kufanya tafiti za Elimu na Maendeleo.
•Amefanya kazi kama Afisa Mratibu wa Utafiti na kuratibu tafiti kubwa zinazofanyika kila Wilaya hapa Tanzania kwa Mikoa ya Shinyanga, Simiyu na Tabora.
•Amesomesha vijana zaidi 1500 katika vyuo vya ufundi( Shinyanga na Mara)na wengi wao hivi sasa wamejiajiri
•Ameajiri vijana 241 waliosomea fani ya elimu, afya, fedha, sheria na maendeleo ya jamii.
AMEIFANYIA NINI TANZANIA?
•Ameshiriki Mijadala Elimishi zaidi ya mia moja, kwenye vyombo vya habari: ITV, TBC, STAR TV, DW, Clouds FM, RADIO One, TBC FM, RADIO Ufaransa, Idhaa ya Kiswahili BBC, na Chanel Ten.
•Ametoa elimu kwa Madiwani Wanawake katika Mkoa wa Shinyanga na Simiyu juu ya kuchambua bajeti yenye mtizamo wa kijinsia.
•Ameendesha semina za mafunzo ya uwajibikaji kwa Maafisa wa Serikali kwenye wilaya 58 za Tanzania Bara.
•Ametoa mada na kushiriki makongamano zaidi ya 30 hapa Tanzania.
•Ameshiriki maadhimisho mbalimbali ya kitaifa
•Ameshirikiana na Serikali na chama cha mapinduzi katika Kutekeleza na kufuatilia utekelezaji wa ilani na mipango ya Serikali kwa mikoa ya Shinyanga, Mara ,Geita, Kigoma na Rukwa.
•Amefadhili na kuratibu fursa za Wanafunzi wengi kwenda ziara ya mafunzo ,kusoma vyuo mbalimbali nchini.
•Ni Mchangiaji mzuri wa shughuli za maendeleo wilaya Rorya na maeneo mbalimbali hapa Tanzania.
ANAAMINI NINI?
Maendeleo huletwa na fikra mpya bunifu zenye kuona mbali.
Hamasa ya utayari wa watu kuthubutu, kuchangamkia fursa za ndani na nje, umakini kusikiliza sauti za wengi na kuchagua vipaumbele sahihi vya mahitaji ya jamii!
INGRI JUU - RORYA
Sanduku la Posta: 250 TARIME
Simu ya Mezani: 0282985583
Simu ya Mkononi :
Barua Pepe za Watumishi: mkurugenzi@roryadc.go.tz
Haki Zote Zimehifadhiwa