MAJUKUMU YA KAZI z IDARA YA MAENDELEO YA JAMII.
1.0 MAJUKUMU YA IDARA:
1.1.Jukumu kuu
Ni kusaidia watu kubadili fikra ,Imani,utamaduni,mila za zamani, zilizopitwa na wakati kuwa zenye mwelekeo wa kimaendeleo.
1.2.Majukumu mahsusi :
• Kuziwezesha jamii kuondokana na fikra, Imani,desturi ,mila na mtizamo unaokinzana na maendeleo.
• Kuziwezesha jamii kutambua fursa walizonazo ili kupanga mipango ya maendeleo nakuziwezesha jamii kuibua, kupanga, kutekeleza, kufuatilia miradi ya maendeleo na shughuli za kujitegemea
• Kujenga uwezo wa halmashauri na vijiji juu ya kutambua, kuunda na kutoa mafunzo kwa vikosi vya ujenzi ili kuwezesha jamii kujiajiri na kuanzisha shughuli za kuongeza kipato
• Kutafsiri na kuelimisha jamii sera mbalimbali
• Kufanya tafiti shirikishi ili kubainivikwazovya maendeleo na matokeo yake kutumika katika kuiwezesha halmashauri kupanga mipango endelevu
• Kuelimisha jamii kuingiza masuala mtambuka katikamipamgo ya maendeleo kama usafi wa mazingira, mapambano dhidi ya rushwa na jinsia.
1. IDARA YA MAENDELEO YA JAMII,JINSIA,WAZEE NA WATOTO:
Shughuli za kufanya:
• Kusimamia utekelezaji wa sera ya maendeleo ya jamii ili kuleta mabadiliko katika jamii kwa kushirikisha wananchi, serikali na mashirika yasiyo ya kiserikali ili kuhakikisha kuwa jamii inakuwa na maendeleo kuanzia mtu mmojammoja familia na jamii kwa ujumla katika Nyanja za kiuchumi,kijamii na kiutamaduni.
• Kusimamia utendaji kazi wa watumishi wote wa sekta yaMaendeleo ya Jamii waliopo wilayani na Katani.
• Kumshauri Mkurugenzi Mtendaji na Idara zenye kuhitaji utaalamu wa masuala ya Maendeleo ya Jamii ,Jinsia wazee na Watoto.
• Kuandaa miongozo ya utekelezaji wa kazi za Maendeleo ya Jamii wilayani.
• Kuwapangia kazi watumishi wa IdaraMaendeleo ya Jamii katika halmashauri.
•
• Kusimamia na kuratibu shughuli zote za makundi maalumu kama vile wazee,walemavu,wanawake ,wajane na vijana kwa ustawi wa Halmashauri.
• Kuelimisha viongozi wa serikali za vijijini,Dini na mashirika yasiyo ya kiserikali kuhusu sera mbalimbali za Wizara ya Maendeleo ya Jamii,jinsia ,wazee na watoto.
• Atawasilisha taarifa za kazi kwa Mkurugenzi Mtendaji na katika vikao vya kamati za kudumu.
2.KITENGO CHA UTAFITI, MIPANGO NA TAKWIMU:
Shughuli za kufanya:
• Kuratibu na kuunganisha taarifa za kazi za idara ya maendeleo ya jamii zinazotekelezwa kutoka katani na vitengo vilivyopo ofisi kuu ya wilaya.
• Kufanya utafiti wa fursa na vikwazo vya maendeleo kwa kutumia mbinu shirikishi kwa kushirikiana na serikali za vijiji.
• Kuandaa miongozo ya utekelezaji wa shughuli za maendeleo ya jamii na kuzisambaza katika ngazi za kata na vijiji.
• Kukusanya takwimu zinazohusu watu na mazingira yao mfano:idadi ya watu,huduma za jamii na kiuchumi zilizopo,kuzichambua,kuzihakiki ,kuzitafsri,kuzitunza , kuzisambaza na kushauri miradi mbalimbali kwa ajili ya matumizi ya halmashauri na jamii kwa ujumla.
• Kuratibu shughuli zote za sehemu ya maendeleo ya jamii na kuziandikia mipango ya utekelazaji.
• Kuandaa mafunzo ya viongozi wa wananchi, watumishi wa maendeleo ya jamii,na makundi mbalimbali katika jamii.
• Kubuni mbinu mbalimbali za kushirikisha wananchi katika mipango ya maendeleo.
• Kufanya utafiti wa awali na utafiti wa kina juu ya miradi inayopendekezwa na wananchi na kutoa taarifa.
• Kuwasaidia wananchi vijijini kuandaa maandiko (project write-ups)ya kuombea fedha za kuendeshea miradi yao.
• Kumshauri mkuu wa idara kuhusu masuala ya maendeleo ya jamii.
• Kuwasilisha kwa mkuu wa idara taarifa ya kazi iliyounganishwa kazi za vitengo vyote na kuhaririwa kulingana na vipindi vya taarifa zinapohitajika.
3.KITENGO CHA MAENDELEO YA WANAWAKE:
Shughuli za kufanya:
• Kuratibu na kufuatilia shughuli za mfuko wa wanawake.
• Kusaidia jamii kuunda vikundi vya kijamii na kimaendeleo.
• Kuhamasisha jamii ili iweze kushiriki katika kazi za kujitegemea.
• Kufanya mapitio ya katiba za vikundi mbalimbali vya kijamii na kufanya marekebisho kwa ajili ya utambuzi.
• Kutambua, Kuratibu kutunza takwimu na kutoa ushauri wa kitaalamu kwa wadau wa maendeleo na Mashirika yasiyo ya kiserikali na kufuatilia utekelezaji wa shughuli zao.
• Kufanya mchakato wa kufuatilia fedha ,kusimamia zoezi la ukopeshaji na ufuatiliaji wa marejesho ya mikopo ya wanawake na kutafuta misaada inayolenga kuleta ukombozi kwa mwanamke.
• Kuratibu utambuzi wa vikundi vya uzalishaji mali na vya kijamii kwa ujumla wake.
• Kumshauri mkuu wa idara kuhusu masuala ya maendeleo ya vikundi na shughuli za uzalishaji mali.
• Kubuni na kusimamia shughuli zinazohusu maendeleo ya wanawake .
• Kuhamasisha na kuwezesha matumizi ya mbinu shirikishi jamii katika kuandaa na kutekeleza mipango ya maendeleo ya halmashauri.
• Kuandaa program za mafunzo kwa vikundi vyauzalishaji mali na utoaji huduma vya kijamii (CBOs) hususani vya wanawake kwa kushirikiana na wadau wa maendeleo ili kuwezesha jamii kutambua fursa zilizopo na kuzitumia kwa maendeleo yao.
• Kuandaa taarifa ya kazi na kuikabidhi kwa mkuu wa idara kwa kila mwezi na kila robo mwaka.
4.DAWATI LA JINSIA NA MAENDELEO YA WATOTO:
Shughuli za kufanya:
• Kuwezesha uingizaji wa masuala ya jinsia katika mipango ya Halmashauri.
• Kuelimisha jamii kuhusu masuala ya usawa wa kijinsia.
• Kukusanya,kuchambua na kuweka takwimu zinazozingatia jinsia zitakazowezesha jamii kupanga mipango yao.
• Kuelimisha jamii juu ya umuhimu wa kutoa taarifa za matukio mbalimbali k.m vifo,milipuko ya magonjwa, masoko, uzalishaji mali,vyakula, ajira na unyanyasaji wa kijinsia.
• Kuwezesha wananchi vijijini kupambana na mila zenye madhara kwa afya za wananchi hasa wanawake na watotowa kike,kuenea kwa virusi vya UKIMWI na magonjwa ya mlipuko.
• Kuhamasisha akina mama wajawazito kuhusu kuhudhuria kliniki na kujifungulia katika vituo vya afya.
• Kuelimisha viongozi wa halmashauri na jamii juu ya umuhimu wa kuzingatia utoaji haki za watoto katika familia.
• Kusimamia sera za maendeleo ya wanawake na watoto katika kupiga vita umasikini na kuondoa suala la ajira kwa watoto.
• Kuandaa habari za mafanikio na matukio mbalimbali ya shughuli za halmashauri na kuziwasilisha kwa Mkurugenzi mtendaji kwa ushauri.
• Kumshauri mkuu wa idara kuhusu masuala ya kijinsia
• Kuandaa taarifa ya kazi na kuiwasilisha kwa mkuu wa idara kila mwezi na kila robo mwaka.
5. URATIBU WA DAWATI LA UWEZESHAJI WANANCHI KIUCHUMI
Shughuli za kufanya:
• Kusimamia na kufuatilia shughuli za uwezeshaji zinazofanywa katika vijiji/mtaa
• Kutafsiri na kusimamia utekelezaji wa sera na sheria ya uwezeshaji wananchikiuchumi na mkakati wa Taifa wa uwezeshaji wanachi kiuchumi katika Halmashauri.
• Kukusanya taarifa na tafiti mbalimbali na kumshauri Mkurugenzi wa Halmashauri katika masuala ya uwezeshaji wananchi kiuchumi na ushiriki wa Watanzania.
• Kuhakikisha fedha za uendeshaji zinatengwa katika bajeti kila mwaka juu ya masuala ya uwezeshaji.
• Kuhakikisha kuwa Halmashauri inahusisha suala la hifadhi ya mazingira na mabadiliko ya tabia ya nchi katika mipango ya maendeleo ya Wilaya ili kuboresha mazingira ambayo ni muhimu katika suala zima la uzalishaji mazao ya kilimo,mifugo na uvuvi.
• Kubuni na kutafuta vyanzo vya rasilimali kwaajili ya shughuli za uwezeshaji katika Halmashauri.
• Kuratibu na kuhamasisha uanzishwaji na uendelezwaji wa vikundi vya kiuchumi kama SACCOS, VICOBA na vinginevyo vinavyosajiliwa na kutambuliwa toka ngazi ya Wilaya hadi Taifa.
• Kuwasilisha taarifa ya utekelezaji kwa kamati ya uwezeshaji ya Halmashauri na baada ya kuidhinishwa itumwe kwa mratibu wa uwezeshaji mkoa na nakala kwa baraza la taifa la uwezeshaji wananchi kiuchumi.
• Kuhamasisha vikundi vya kijamiina kiuchumi kijisajili/kujirasimisha na kufanya uzalishaji wenye viwango kama vya TBS, TFDA na kupata nembo ya utambuzi wa bidhaa (msimbomilia) (barcode)
• Kuandaa taarifa ya maendeleo ya vyama vya ushirika hasa SACCOs na vikundi vya kiuchumi kama VICOBA vilivyopo katika Halmsahauri.
• Kubuni fursa mbalimbali za uwekezaji katika Halmashauri.
• Kufuatilia upatikanaji wa masoko ya bidhaa za kiuchumi.
• Kushauri namna ya uboreshaji wa vituo vidogovidogo vya kibiashara katika vijiji na mamlaka za miji midogo.
• Kuhakikisha Halmashauri inatoa kipaumbele (preferential treatment) kwawatanzania hasa wakazi wa kwenye Halmashauri katika utoaji wa zabuni.
• Kutoa taarifa ya mwezi ,robo mwaka na kuiwasilisha kwa mkuu wa idara
6. URATIBU WA UKIMWI WA HALMASHAURI
Shughuli za kufanya:
• Kuratibu na kusimamia shughuli za mwitikio dhidi ya VVU/UKIMWI katika Halmashauri.
• Kushirikiana na wadau (asasi na watu wanaoishi na VVU) kutengeneza mpango wa Halmashauri wa mwitikio wa VVU na UKIMWI.
• Kuelimisha jamii juu ya mbinu za kujikinga dhidi ya maambukizi mapya ya VVU kwa kutumia njia mbalimbali kama Sanaa shirikishi, sinema, semina, warsha nk.
• Kuratibu ukusanyaji na utunzaji wa takwimu za huduma za VVU/ UKIMWI kupitia mfumo wa TOMSHA.
• Kuimarisha shughuli za kiuchumi kuongeza kipato kwa watu wanaoishi na virusi vya UKIMWI.
• Kubuni vyanzo vya mapato ili kutunisha mfuko wa mwitikio wa VVU/UKIMWI.
• Kutoa misaada kwa makundi, familia na watoto wanaoishi katika mazingira hatarishi,kutegemea na upatikanaji wa rasirimali.
• kuandaa taarifa ya kazi na kuikabidhi kwa mkuu wa idara kila mwezi na kila robo mwaka.
7. KITENGO CHAUJENZI NA UFUNDI:
Shughuli za kufanya:
• Kuwezesha jamii kushiriki katika kubuni,kupanga,kutekeleza,kusimamia, kutathmini mipango/miradi ya maendeleo .
• Kuhamasisha na kuwawezesha wananchi kupanga na kutekeleza kazi za maendeleo ambazo ni pamoja na usafi na utunzaji wa mazingira,ujenzi wa nyumba bora vijijini,ujenzi wa shule,zahanati,majosho,barabara za vijijini (feeder Roads),uchimbaji wa visima na malambo.
• Kuandaa ramani za nyumba bora zinazotumia teknolojia rahisi gharama nafuu.
• Kuwawezesha wananchi kubaini na kuratibu rasilimali zilizopo na kuzitumia katika miradi ya kujitegemea.
• Kuhamasisha jamii na kuwawezesha kuona umuhimu wa kuthamini mazingira kwa kutumia nyenzo sahihi na rahisi zinazosaidia kuhifadhi na kuendeleza mazingira na vyanzo vya maji.
• Kuandaa na kusimamia mafunzo ya teknolojia rahisi na sahihi.
• Kuwashauri wakuu wa idara zenye miradi ya ujenzi kuhusu masuala ya shughuli za ufundi na ujenzi.
• Kuandaa taarifa ya kazi na kuikabidhi kwa mkuu wa idara kila mwezi na kila robo mwaka.
8.KITENGO CHA VIJANA
Shughuli za kufanya:
• Kushirikiana na wataalam wa sekta ya maji katika kufanikisha mipango ya maendeleo ya sekta hiyo kwa kuongeza kasi ya ushiriki wa jamii.
• Kuwahamasisha na kuwawezesha wananchi kulinda na kuhifadhi vyanzo vya maji
• Kuratibu na kufuatilia shughuli za mfuko wa maendeleo ya vijana
• Kuratibu na kusimamia utekelezaji wa sera ya vijana
• Kuhamasisha vijana kufufua moyo wa kujitolea kwa ajili ya maendeleo yao na jamii kwa ujumla.
• Kupanga na kuendesha mafunzo yanayohusu stadi za kazi na afya ya uzazi kwa vijana
• Kuanzisha vituo vya ushauri nasaha,elimu ya familia na ajira kwa vijana kwa kushirikiana na ASASI za kiraia.
• Kukusanya,kutunza na kuzisambaza taarifa mbalimbali zinazohusu vijana
• Kuhamasisha vijana kuunda vikundi vya ujasiriamali
• Kuwaunganisha vijana kutumia fursa zilizopo katika maeneo yao na kuwaunganisha na taasisi za kifedha zilizopo ili waweze kupata mikopo.
• Kuandaa taarifa ya kazi na kuikabidhi kwa mkuu wa idara kila mwezi na kila robo mwaka.
INGRI JUU - RORYA
Sanduku la Posta: 250 TARIME
Simu ya Mezani: 0282985583
Simu ya Mkononi :
Barua Pepe za Watumishi: mkurugenzi@roryadc.go.tz
Haki Zote Zimehifadhiwa