1.UTANGULIZI
Halmashauri ilipokea fedha Kiasi cha Tsh. 584,280 028.00 (Milioni mia tano themanini na nne mia mbili themanini elfu na ishirini na nane tu) kupitia Akaunti ya Shule ya Sekondari Mirare ili kutekeleza Ujenzi wa Shule mpya ya Sekondari Ingri kupitia fedha za Serikali Kuu -Mradi wa SEQUIP.
Baada ya kukiri kupokea fedha hizo na kuwajulisha wajumbe wa Bodi ambao waliunda Timu ya Usimamizi na utekelezaji wa mradi, timu ya manunuzi pamoja na timu ya ukaguzi na mapokezi ya vifaa.
Eneo la mradi
Mradi huu unatekelezwa katika Kata ya Mirare Kijiji cha Ingri Juu.
Thamani ya mradi
Mradi huu una thamani ya Tsh 584, 280,028.00 ambazo zimetokana na SEQUIP, ambazo zimegawanyika kwenye mjengo mbalimbali kama ifuatavyo:
Jengo la utawala – 77,708,333.00/=
Madarasa 02 bila ofisi – 100,000,000/=
Madarasa 02 na ofisi – 109,378,850
Maabara kemia na biolojia 102,000,000/=
Maabara ya fizikia – 51,000,000/=
Maktaba – 61,922,982.000/=
Chumba cha Tehama – 51,044,864.00/=
Vyoo vya wavulana – 10,500,000/=
Vyoo vya wasichana – 12,600,000/=
Kichomea taka – 4,166,667.00/=
Tank la ardhini – 3,958,333.00/=
Mradi huu ulianza 25,08.2023 kwa kuanza na ufyatuaji wa tofali za block inch 6. Ujenzi wa msingi wa majengo ulianza rasmi tarehe 01.09.2023 na tunatarajia kukamilisha ifikapo tarehe 31.10.2023.
Mradi huu una awamu moja tu kwa mwaka wa fedha 2022/2023.
KIASI KILICHOTUMIKA MPAKA SASA
Fedha ambazo zimeshalipwa kutoka kwenye akaunti ni Tsh 234,610,000/= na deni yavifaa vya ujenzi ambazo zipo kwenye eneo la mradi ni Tsh 104,571,000/= ambazo mchakato wa malipo yake unaendelea. Jumla ya matumizi ni Tsh 339,181,500/=
KIASI AMBACHO HAKIJATUMIKA
Mpaka sasa kiasi cha Tsh 245,098,528/= bado hakijatumika na kipo kwenye akaunti ya shule ya sekondari Mirare.
INGRI JUU - RORYA
Sanduku la Posta: 250 TARIME
Simu ya Mezani: 0282985583
Simu ya Mkononi :
Barua Pepe za Watumishi: mkurugenzi@roryadc.go.tz
Haki Zote Zimehifadhiwa