Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Rorya. Ndugu Charles K. Chacha, Anawatangazia wananchi wote kuwa kutakuwa na Maadhimisho ya siku ya Wanawake Duniani 8/3/2018 na Maadhimisho hayo yataenda sambamba na Juma la maonesho ya shughuli za kiuchumi zinazofanywa na Wajasiriamali wanawake Wilayani Rorya katika kuelekea Uchumi wa Viwanda. MAADHIMISHO YATAFANYIKA KATIKA VIWANJA VYA OFISI YA MKUU WA WILAYA YA RORYA.
KAULIMBIU YA SIKU YA WANAWAKE DUNIANI KWA MWAKA 2018 INASEMA "KUELEKEA UCHUMI WA VIWANDA, TUIMARISHE USAWA WA JINSIA NA UWEZESHAJI WA WANAWAKE VIJIJINI"
INGRI JUU - RORYA
Sanduku la Posta: 250 TARIME
Simu ya Mezani: 0282985583
Simu ya Mkononi :
Barua Pepe za Watumishi: mkurugenzi@roryadc.go.tz
Haki Zote Zimehifadhiwa