Kamati ya Michezo (Wilaya) inawatangazia Wananchi wa Rorya hususan wa Shirati na Maeneo ya Jirani kuwa Kutakuwa na Ufanyaji wa Mazoezi yatakayohusisha Wananchi Wote na Wafanyakazi Wote Katika Uwanja wa Mpira wa Miguu SHIRATI OBWERE.
Mazoezi hayo yatafanyika tarehe 13 Mei 2017, Siku ya Jumamosi kuanzia saa 1:30 Asubuhi.
Huu ni Utekelezaji wa Agizo la Makamu wa Rais wa Tanzania, Mh. Samia H Suluhu wa kufanya mazoezi kila Jumamosi ya Wiki ya pili ya kila Mwezi.
KARIBUNI SANA, MAZOEZI HUONDOA MAGONJWA YA KISUKARI, SHINIKIZO LA DAMU NA HUIMARISHA AFYA NA AKILI.
INGRI JUU - RORYA
Sanduku la Posta: 250 TARIME
Simu ya Mezani: 0282985583
Simu ya Mkononi :
Barua Pepe za Watumishi: mkurugenzi@roryadc.go.tz
Haki Zote Zimehifadhiwa