Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Rorya. Anawatangazia wananchi wote Tarehe 16.01.2018 siku ya Jumanne Waziri Mkuu Mheshimiwa Kassim Majaliwa Majaliwa (Mb) atatembelea Wilaya ya Rorya na atafanya ziara ya kikazi ya siku moja. Akiwa Wilayani Rorya, Waziri Mkuu atafanya shughuli mbalimbali za kiserikali zikiambatana na kukagua na kutembelea baadhi ya miradi ya maendeleo na kuongea na kuhutubia mkutano wa hadhara kwa wananchi wa Rorya ambao utafanyika katika kijiji cha Bubombi, Kata ya Bukura.
INGRI JUU - RORYA
Sanduku la Posta: 250 TARIME
Simu ya Mezani: 0282985583
Simu ya Mkononi :
Barua Pepe za Watumishi: mkurugenzi@roryadc.go.tz
Haki Zote Zimehifadhiwa