Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Rorya Ndg. Charles K Chacha amefungua Mafunzo ya Siku Mbili ya Mfumo wa Uhasibu na Utoaji Taarifa za Fedha kwa Ngazi ya Kituo cha Kutolea Huduma (Facility Financial Accounting and Reporting System ''FFARS'' kwa Waratibu Elimu Kata, Wakuu wa Vituo vya Afya na Mhasibu wa Hospitali ya Wilaya. Mafunzo hayo yanafanyika katika Ukumbi wa SOA, Utegi-Rorya kuanzia tarehe 12 hadi 13, Jumi 2017, na baadaye Washiriki hawa Kusambaa Wilaya nzima kupeleka Mafunzo hayo kwa Walimu Wakuu Shule za Misingi, Wakuu wa Shule za Sekondari na Wakuu wa Zahanati.
Akifungua mafunzo hayo, Mkurugenzi Mtendaji aliwasihi Washiriki Wote wa Mafunzo Kuhakikisha wanasikiliza kwa makini ili mafunzo haya yakapate kuwa na tija kwa Kuwaondolea Usumbufu wa Ukaguzi wa Kifedha na kuleta Urahisi na Usahihi wa Kuripoti Taarifa za Fedha.
Malengo ya Mfumo huo kwa Washiriki wa Mafunzo hayo kuwajengea uwezo watoa huduma katika vituo vya kutolea huduma, kusaidia upatikanaji wa taarifa sahihi katika mahesabu ya mapato na matumizi ya halmashauri na kuunda kusaidia kuhakikisha fedha za ruzuku zinasimamiwa vizuri na taarifa za matumizi yake zinatolewa kwa usahihi tofauti na ilivyokuwa mwanzo.
Mfumo huo wa FFARS unatekelezwa kwa ushirikiano baina ya Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI), Wizara ya Fedha na Mipango, Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi na Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, pamoja na Mradi wa Kuimarisha Mifumo ya Sekta za Umma (PS3) unaofadhiliwa na Shirika la Misaada la Watu wa Marekani (USAID).
INGRI JUU - RORYA
Sanduku la Posta: 250 TARIME
Simu ya Mezani: 0282985583
Simu ya Mkononi :
Barua Pepe za Watumishi: mkurugenzi@roryadc.go.tz
Haki Zote Zimehifadhiwa